PAC yaibua ufisadi mwingine
Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) imeanika
madudu na kashfa za kutisha katika ripoti maalumu ya
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG),
ikiwa ni pamoja na zaidi ya Sh100 bilioni kukwepwa
kulipwa na kampuni mbalimbali kwa kivuli cha
misamaha ya kodi.
Ripoti hiyo iliyowasilishwa jana na Mwenyekiti wake,
Zitto Kabwe imeeleza ukiukwaji wa Sheria ya Ununuzi
wa Umma, jinsi ujenzi wa jengo la watu mashuhuri (VIP)
katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu
Julius Nyerere, Dar es Salaam (JNIA), ulivyofanyika bila
kibali kutoka Baraza la Mawaziri, huku mchango wa
ujenzi wa jengo hilo kwa Serikali ukiongezwa kwa Sh2.3
bilioni.
Source:mwananchi comm.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni